KONYAGI

KWA MATANGAZO PIGA SIMU NAMBA (+255) 0758474500

IDADI YA WAGENI

jiunge na chekanakitime group ya whatsapp

Jiunge na WhatsApp group ya Chekanakitime - +255758474500

leta tucheke

leta tucheke

FUATILIA KWENYE FACEBOOK

August 21, 2014

MAFALA WAKO WENGI


Posted By John KitimeThursday, August 21, 2014

VICHWA VYA HABARI

 Wahezaji?

 Umeona ee tumeendelea sana, tunacheza kwa kutumia umeme

 Wanawake wenzio watapumua sasa

DUH

Posted By John KitimeThursday, August 21, 2014

MWALIMU KASEMA TUJIHESHIMU

MAMA: We mtoto mbona kila asubuhi unajiangalia kwenye kii harafu unajiamkia shkamoo?
DOGO: Mwalimu kasema lazima tujiheshimu

Posted By John KitimeThursday, August 21, 2014

August 20, 2014

ZAMU YAKO NIFUKUZE NA MIMI

Mgonjwa kwenye hospitali ya machizi alikuwa kaokota kisu, akaanza kumfukuza daktari mmoja kisu mkononi macho yamemtoka kwa hasira, daktari kapaniki akakimbia hatimae akafika kwenye geti akakuta limefungwa akasimama akiwa amekata tamaa, chizi akaja spidi na kisu kanyanyua, alipofika kwa daktari akashusha kisu;
CHIZI: Haya sasa zamu yako chukua kisu anza kunifukuza na mimi

Posted By John KitimeWednesday, August 20, 2014

NIMEMPA MATONE YA DAWA YA MACHO

Dokta mmoja alikuwa amepata dharula akamwambia mlinzi wa hospitali yake ahakikishe hospitali inabaki wazi. Baada ya masaa mawili akarudi;
DOKTA: Vipi hapa salama?
MLINZI: Salama tu mzee,  alikuja jamaa mmoja akasema anaumwa kichwa nikampa panadol
DOKTA: Safi sana
MLINZI: Akaja mwingine akasema anaumwa tumbo nikampa flajil
DOKTA: Aise we mkali safi sana
MLINZI: Wakati nataka kufagia ofisi amekuja binti mmoja mzuri sana wa Bongomuvi kaingia fosi kavua nguo zote, kapanda kwenye kitanda cha kupimia wagonjwa kalala, akaniambia, nimsaidie hajamuona mwanaume mwezi wa sita na hawezi kuvumilia zaidi, basi nikamnyunyizia machoni matone ya dawa ya macho
DOKTA: Duh

Posted By John KitimeWednesday, August 20, 2014

HAYA NINONG'ONEZE SIKIONI...........

Dogo alikuwa kanisani na mama yake, mkojo ukambana;
DOGO: Mama mi nataka kukojoaaa
MAMA DOGO: Nyamaza ukiwa kanisani usiwe unasema unataka kukojoa sema nataka ninong'one, mi ntaelewa unasikia wewe?
Wiki inayofuata Dogo akaenda kanisani na baba yake, ghafla;
DOGO: Baba mi nataka ninong'one
BABA DOGO: Haya ninong'oneze sikioni

Posted By John KitimeWednesday, August 20, 2014

August 19, 2014

NDIO LAZIMA TUPATE KATIBA MPYA

Jamaa alikuwa kakaa kiti cha nyuma kabisa kwenye daladala, pembeni yake kuna binti mzuri akaanza kumpa maneno matamu, binti akawa anamkatalia, jamaa hakukata tamaa , na binti hakubadili mawazo, hatimae binti akawa amekasirika, akamwambia jamaa kwa ukali na sauti ya juu basi zima wakasikia,'We baba vipi? Kwani lazima?" Jamaa akajibu nae kwa nguvu, 'Ndio ni lazima tupate Katiba mpya maana hii ya sasa imepitwa na wakati'

Posted By John KitimeTuesday, August 19, 2014

BEFORE AND AFTER


Posted By John KitimeTuesday, August 19, 2014

NDUGU MHARIRI NINA TATIZO

Ndugu Mhariri wa Blog naomba msaada.
Mimi ni mke wa mtu. Mume wangu ana miaka 40 mimi nina miaka 36, maisha yetu kwa kweli ni mazuri na yalikuwa na raha mpaka baada ya tukio ntakalo hadithia. Leo asubuhi niliamka kuwahi kazini nikamuacha mume wangu na msichana wa kazi nyumbani, mume wangu alinambia kuna kazi anafanya nyumbani kabla ya kwenda kazini kwake. Nimeondoka na moja ya gari zetu tatu sikufika mbali gari ikaanza kuchemsha  hivyo nikalazimika kurudi kubadilisha gari. Nimefika kwangu  nimemkuta mume wangu chumbani kwetu na msichana wa kazi , nimechanganyikiwa naomba ushauri, nifanye nini?
Mama Siwema.
JIBU
Mama Siwema ,
Kwa kweli umetumia busara sana kuuliza nini cha kufanya. Mimi kama mhariri wa Blog hii nakusifu kwa umakini wako na pia kukusifu kwa kujua wazi swala gumu kama hilo jibu lake litaweza kupatikana kupitia blog hii makini. Sasa tuanze na chanzo cha tatizo.  Gari lako lilianza kuchemsha, hii ni wazi kuwa aidha maji yameisha kwenye redieta, au redieta inavuja, au uliwahi kutembea bila maji sasa silinda hed imepinda. Ushauri ni kuwa ni vizuri upeleke gari kwa  fundi. Kuna jamaa pale Mwananyamala anaitwa Fundi Hamisi huyu ataweza kukutatulia tatizo bila wasiwasi yuko nyuma ya soko , we ulizia tu fundi Hamisi watakuonyesha gereji yake. Nategemea jibu hili litakuwa limekumalizia tatizo lako 
Aksante
Mhariri

Posted By John KitimeTuesday, August 19, 2014

JE NI KWELI? AU THI KWELI?

Kwa muda mrefu kumekuwa na stori kuwa wale jamaa dhetu wanaoishi karibu na Moshi huwa wanakula ugali kwa picha ya thamaki. Blogu yenu tata ilituma timu ya wapelelezi kwenda kufukunyua kuhusu hili. Nyumba ya kwanza kuingia tu, wapelelezi wetu walikaribishwa msosi huu laiv. Bado ushahidi hautoshi upelelezi unaendelea

Posted By John KitimeTuesday, August 19, 2014

MKE WANGU MIMI KAZI BASI

Mke alikuwa kaenda mjini kwenye shughuli zake ghafla akapata wazo amtembelee mumewe ofisini. Ile kufungua mlango wa ofisi ya mumewe si kamkuta sekretari kamkalia mumewe pajani. 
MUME: Karibu mke wangu mpenzi karibu. Unajua mimi sasa kazi kwenye kampuni hii nimeshindwa, hebu ona wamebana matumizi wanatuambia wafanyakazi wawiliwawili tutumie kiti kimoja na kompyuta moja. Yaani nilikuwa nirudi leo nikwambie kuwa mimi kazi basi tuangalie mbele yajayo.

Posted By John KitimeTuesday, August 19, 2014

August 16, 2014

MUUJIZA YULE DADA ALIYEKUFA KAFUFUKA

MKE: Ulilala wapi? Unadharau sana unanirudia mie alfajiri, leo lazima unambie huko ulikolala
MUME: Mke wangu mpenzi jana nilichanganyikiwa, si unamfahaamu rafiki yangu Joshua, basi jana dadake kaanguka kafariki ghafla basi nimelazimika kulala huko kumliwaza
MKE: Ok naoga na mie nikawape pole........(akaenda kuoga)
MUME: Yaani maajabu makubwa yametoea, muujiza laiv
MKE: Kivipi?
MUME: Ulipoenda kuoga, Joshua kanipigia simu eti kuna mchungaji kaja kumuombea yule dadake aliyekufa sasa kafufuka hivyo wameondoka kuelekea kijijini kwao kuwaona wazazi wao, yaani muujiza

Posted By John KitimeSaturday, August 16, 2014

KUNA LIMBABA LINANIBAKA..........


Mdada aliyekuwa anabakwa akafanikiwa kuishika simu yake, akapiga simu polisi;
POLISI: Haloo polisi hapa tukusaidieje?
MDADA: Polisi nisaidieni, kuna libaba linanibaka, nisaidieni mje mlikamate kesho

Posted By John KitimeSaturday, August 16, 2014

NAKEMEA PEPO LIKUTOKE

MCHUNGAJI: Nakemea pepo la wizi likutoke
MUUMINI: Amen
MCHUNGAJI: Nakemea pepo la uwongo likutoke
MUUMINI: Amen
MCHUNGAJI: Nakemea pepo la uasherati likutoke
MUUMINI: Ngoja kidogo mzee, hilo utalikemea kesho

Posted By John KitimeSaturday, August 16, 2014

ANGALIA TEMBO WAKIKATA NYONGA -VIDEO

video

Posted By John KitimeSaturday, August 16, 2014

TUMEYAONA MAGALIZETINI

Hii kali Wahehe na wamasai ruksaaaaaa.
_______________     _________________  _________


TUMEINYAKA TOKA GAZETI FUDENGE........Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu kubwa ya mapaja wazi, wanaume wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu......MJI WA NAIVASHA ULIOPO NAIROBI.....TEH TEH TEH TEH

Posted By John KitimeSaturday, August 16, 2014

HATARI HATARI WIZI MPYA WAINGIA MJINI.......TAKE CARE

Blogu yenu siriaz ingependa kuwataarifu wasomaji wote kuhusu wizi mpya ambao unaendelea mjini. Wizi huu hufanywa na vibinti vinavyovutia sana, na wanaume tu ndio huibiwa, hivyo akina mama tafadhali muwambie waume zenu na maboifrend wajihadhari. Wizi huu hutokea kule baharini maeneo ya Koko, ukipaki tu vibinti viwili vizuri huja na kuanza kusafisha kioo cha gari lako, wakati wakifanya hivyo hujiachia viblauzi na visidilia vyao unajikuta huwezi kuacha kukodolea macho. Vikimaliza usafi husema havihitaji malipo ila vinaomba lifti kwenda Msasani. Ukikubali vinapanda kiti cha nyuma na kuanza kukushika shika shingo na masikio, kamoja kanahama kiti na kuja kiti cha mbele na kuanza kukula denda wakati kenzie kanakuibia mkwanja wako. Bosi wetu kaibiwa juzi, jana tena kaibiwa na leo keshatupigia simu kuwa kaibiwa, na kesho ni wazi ataibiwa. Tunaomba mjihadhari sana
Aksante

Posted By John KitimeSaturday, August 16, 2014

August 14, 2014

WAKUBWA WAZIMA MNAAMINI MAZIMWI


Mheshimiwa mmoja baada ya kupata cheo si akapewa nyumba mitaa ya watu wenye pesa, akahamia huko akiwa na mke na mwanae. Siku moja mwanae aliyekuwa kazoea maisha ya Uswazi akawa anawinda ndege na manati kwenye uwanja wa jumba lao, bahati mbaya jiwe likapitiliza na kwenda kuvunja kioo cha nyumba ya jirani. Mheshimiwa na mkewe wakaamua kumfuata mwenye nyumba wakamuombe msamaha. Walipogonga mlango akafukua mbaba mmoja akawakaribisha kwa heshima, wakaingia na kuanza kujieleza. ‘Samahani sie tumehamia karibuni hapo nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo chako kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha na kuona kama tunaweza kutengeneza’. Mwenyeji wao akawaomba wakae  kisha akawaambia, ‘Naomba niwahadithie kitu. Kwanza mimi nawashukuru nyinyi na mtoto wenu. Mwenye nyumba hii ni mchawi mkubwa sana, mimi ni ZIMWI alikuwa amenifungiwa kwa zaidi ya miaka 200 kwenye kichupa ambacho kilikuwa kwenye  dirisha lililovunjwa na chupa nayo ikavunjika nami nimekuwa huru, kwa hiyo kwa shukurani ombeni chochote mtakacho nitawapa, nina uwezo huo’ Hapo hapo muheshimiwa akauliza tena,’Yaani kitu chochote?’ Akajibiwa ‘Ndio’. Basi pale pale akasema, ’ Mimi naomba niwe bilionea mpaka nife’ Akajibiwa ,’ Hilo jambo dogo sana kwangu, umepata na kesho utaamka tajiri’ Mama nae akaomba vyake, ‘Mi nataka niwe na nyumba kila nchi duniani na niwe na biashara Dubai na China na HongKong’ Akajibiwa, ‘Umepata mama, kuanzia kesho hayo ni yako. Mimi nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina kaombi kadogo’. Mheshimiwa haraka akajibu, ’Sema tu wewe ni kama ndugu yetu sasa’ Basi ZIMWI likasema, ‘Naomba mkeo abaki hapa kama masaa mawili tu, unajua kifungo nilichofungwa kilinizuia kila kitu, hata mke sijapata kipindi chote hicho. Nikimaliza tu hilo ntaondoka kurudi kwetu Uzimwini hamtaniona tena, itakuwa siri yetu’. Mme na mke wakajadiliana wakaona utajiri waliopata ni mkubwa sana, na hilo jambo ni dogo sana la mara moja tu tena kwa siri, wakakubali sharti. Mke akabaki pale kwa masaa kadhaa.  Shughuli ilipokwisha, mama wa watu akiwa anajitayarisha kurudi kwa mumewe kichwani akiwaza utajiri, ZIMWI likakohoa kidogo na kumuuliza yule mama, ‘Samahani una miaka mingapi na mumeo ana miaka mingapi?” Mama wa watu akajibu, ‘Mie nina miaka 40 mume wangu ana miaka 46’ Yule Mbaba akacheka sanaa, ‘Sasa nyinyi wakubwa wazima mpaka leo mnaamini stori za MAZIMWI?

Posted By John KitimeThursday, August 14, 2014

August 9, 2014

THE SPIRIT OF THE NATION


KAUNTA YA JUMAMOSI

Posted By John KitimeSaturday, August 09, 2014

NAGAWA FRIJI BURE KARIBUNI

BOSI wetu alinunua friji jipya, akawaza namna ya kuondokana na lile la zamani lililokuwa bovu na haliuziki, basi akaliweka nje ya nyumba yake na kuandika kibao ANAE TAKA KUCHUKUA ACHUKUE BURE, watu wakawa wanapita wanafungua lakini kila mtu akawa anaogopa kuchukua maana hakuna aliyeamini mtu anaweza akagawa friji zima bure. Baada ya kuona wiki imepita halijachukuliwa, akaandika FRIJI INAUZWA LAKI 3, usiku uleule likaibiwa

Posted By John KitimeSaturday, August 09, 2014

WACHEKAJI WA ZIADA

MABOSI WA HII BLOGU

WANAOPENDA KUCHEKA

UA-35416264-1